Burna Boy Kutumbuiza Katika Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya
Miezi michache iliyopita mwanamuziki kutokea Nigeria Davido alifanikiwa kuwa moja kati ya wasanii waliotumbuiza katika michuano ya Kombe la Dunia na sasa ni zamu ya Burna Boy, kwenda kukiwasha katika fainali za ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kupitia video fupi aliyoisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilimuonesha mkali huyo wa midundo ya AfroFuse akiutangazia umma juu ya kutumbuiza katika fainali hizo.
SOMA PIA: Navy Kenzo Waachilia Albamu Mpya
Katika video hiyo fupi, The African Giant alianza kwa kuwasalimia mashabiki wake kisha kuwapatia taarifa hiyo njema ya kuhusika kwa kusema
Hello Everyone, This is Burna Boy and I got some big News I will be Performing at the UEFA Champions league finals kick off show by Pepsi. COME ON LET GO.
Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitafanyika nchini Uturuki katika jiji la Istanbul mwezi Juni.
Burna pia kwa mwaka huu amefanikiwa kutumbuiza jukwaa la NBA all Star Game akiwa na wasanii wengine kama vile Tems pamoja na Rema