Home » KRG The Don Afichua Chanzo Chake Cha Utajiri

Rapa na mfanyabiashara wa Kenya KRG the Don amefichua chanzo chake cha utajiri.

 

Akizungumza katika mahojiano na podcast ya Iko Nini, KRG alisema nyanyake alimwachia urithi kabla hata hajafikisha miaka 18.

 

“Babu yangu alifariki siku 30 kabla sijazaliwa. Alisema mtoto wa pili aliyembeba mama ndiye atakayerithi mali yake. Ni mimi hivyo nyanya yangu alipofariki mwaka 2007 aliita kila mtu na kutangaza mali yote iliyobaki akanipa”.

 

KRG pia alifichua kuwa alikuwa na kandarasi ya kusambaza ballast na mchanga wakati wa ujenzi wa SGR kutoka 2014 hadi 2016 na pia alitengeneza pesa nzuri kutokana nayo.

 

Katika mahojiano ya awali, rapper huyo alisema familia yake iliona uwezo wake na iliwekeza kwake kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

 

“Baba yangu alikuwa akinipa pesa nyingi, alikuwa akinipa kama Sh150,000 na nilihitaji Sh40,000 pekee. Nilikuwa na bidii na niliitumia kwa busara.”

 

Mnamo Oktoba mwaka jana, KRG the Don alifichua kuwa thamani yake ni  Bilioni 5. Akizungumza wakati wa mahojiano na Dk.Ofweneke kwenye Tv 47, mwanamuziki huyo alisema utajiri wake umekua kwa miaka mingi na kuongeza kuwa alitengeneza milioni yake ya kwanza mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 17.

 

Alisema amewekeza katika biashara ya majengo, usafiri na muziki.

 

Alisema kwa yeyote anayetilia shaka utajiri wake atoe taarifa kwa mamlaka yoyote kwa kuwa yuko tayari kutoa hesabu ya fedha zake.

 

Msanii huyu wa Dancehall anajulikana kwa mtindo wake wa maisha ya kifahari na huwa mwepesi wa kujivunia utajiri wake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!