Zari Awahakikishia Wanawe Maisha Mazuri

Sosholaiti wa Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Zari Hassan amesambaza video yenye hisia kali ya wanawe wakitembelea kaburi la baba yao.
Ivan Ssemawanga alifariki dunia mwaka 2017 baada ya kuugua ugonjwa wa moyo na aliwaacha watoto watatu na Zari.
Katika Instagram stories, Zari ameeka video ya wavulana wake wakiwa wametembelea kaburi huku wakionekana kufadhaika na hisia tele.
Mama wa watoto watano aliwafariji, na kuwahakikishia kwamba kila kitu kitakuwa sawa.
Zari amewapiga vijembe wanawake waliokuwa wamemfikia wakiomba kuunganishwa na wanawe. “Sitawahi kuwaambia wanangu nani wa kuchumbiana, au ni msichana yupi sahihi kwao, wachumbie wamtakaye, ninachoweza kufanya ni kuwashauri kuhusu maisha, hilo ndilo ninaloweza kufanya kama mama. kwa hakika wanawake hao watakuwa na bahati ya kuwa na mama mkwe mzuri.”
Zari anapenda kujivunia jinsi alivyowalea vizuri watoto wake akisema wana tabia nzuri, warembo, na bila shaka matajiri.
Zari alifichua kuwa Pinto anawajibika na amekomaa. Yeye pia ndiye mrithi halali wa biashara kubwa. Alitangaza kwamba atachukua biashara ya familia. Familia hiyo inasemekana kumiliki chuo na biashara nyinginezo nchini Afrika Kusini.
Baada ya kifo cha Ivan, Zari aliendelea na kufunga ndoa na supastaa wa Tanzania Diamond Platnumz.
Hata hivyo, ndoa yao ilishindwa na wakaachana. Wamekuwa wazazi pamoja kwa amani kufikia sasa.
Sasa Zari anamchumbia Shakid Lutaayo na Wanandoa hao wamekuwa wanalaumiwa kwa sababu Zari ni mkubwa kuliko Lutaayo.
Sosholaiti huyo alibainisha kuwa maisha yake ya mapenzi ni maamuzi yake na kwamba hakuna mtu aliye na mamlaka ya kuhoji maamuzi yake au washirika anaowachagua.
“Bitches, mimi sio mpenzi wa kung’ang’ania, hiyo ni tabia ya mpenzi tu, Mbona unapata hisia kama niko juu ya mtu wangu, sio mtu wako, mtu wangu?