Home » Marioo, Romy Jons Waacha Ujumbe Mzito

Marioo aacha ujumbe mzito

Mwandishi na muimbaji wa nyimbo za  Bongo Fleva Omary Mwanga  ambaye pia anajulikana kwa jina la Marioo, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameacha ujumbe mzito kwa jamii.

 

 

Katika ujumbe huo Marioo ameandika juu ya kifo na kutenda wema kwa kusema:

 

“Kwa sababu sisi sote hii dunia tutaiacha tena kwa namna ambayo hatujui ni dakika ya ngapi, Ndo mana me sitamani kuwa na shida na mtu, kufanya kila kitu kinachowezekana in a good way wala sio ujinga”

 

Mbali na Marioo, DJ na Mwanamuziki Romy Jons naye hayaacha kuandika juu ya hisia zake kwa wale walitutangulia mbele za haki kwa kuandika

 

 

……TUSALI NA KUWAOMBEA WALIOTUTANGULIA IN SHA ALLAH….AND KEEP FIGHTING FOR OUR DREAMS NO ONE KNOWS TOMORROW….

Romy jons

SOMA PIA:Mastaa Bongo Waomboleza Kifo Cha Costa Titch

 

Vifo viwili  vilivyojitokeza nchini Afrika ya Kusini vikiwagusa wasanii mashuhuri wa muziki wa nchi hiyo ni kifo cha AKA pamoja na Costa Titch vilivyoleta gumzo la hali ya juu katika nchi hiyo na hata kwa watu wa mataifa mengine.

 

Juu ya vifo hivyo, huenda ndiyo sababu iliyompelekea mshindi huyo  wa Tanzanian Music Awards kuandika ujumbe huo wenye maana kubwa kwa jamii na watu maarufu wote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!