Home » Mastaa Bongo Waomboleza Kifo Cha Costa Titch

Badaa ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha mwanamuziki kutokea Afrika ya Kusini Costa Titch (28), baadhi ya mastaa wa bongo wameomboleza kifo cha nyota huyo.

Baadhi ya Nyota hao ni pamoja na mwanamuziki Nasib Abdul  almaarufu Diamond Platnumz, ambaye kwa upande wake amefikia hatua ya kutumia ukurasa wake wa Instagram kusambaza picha za Costa Titch.

 

 

Mbali na Diamond pia mwanamuziki mwingine ni Marioo ambaye kupitia akaunti yake ya Twitter aliichapisha picha ya Costa na kuandika RIP Costa gone too soon

 

Pia muigizaji Wema Sepetu ameonesha hisia zake za kuumizwa na kifo hicho huku opia kupitia ukurasa wa Instagram akiandika… This is sad…..RIP Costa Titch…..Gone too soon..

 

 

SOMA PIA:Wafahamu Washindi Wa Tuzo Za Orange

 

Kifo cha Costa Titch ni pigo kwa wadau na mashabiki wa muziki haswa kutokea Afika ya Kusini kwa kuwa hili ni pigo lingine baada ya kifo cha AKA kilichozua taharuki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!