Home » Frida Kajala Azungumzia Mahusiano Na Harmonize Baada Ya Kutemana

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Frida Kajala Masanja anaonekana kuendelea vizuri na hadhi yake mpya ya mahusiano ikiwa ni miezi michache baada ya kuachana na bosi wa kundi la Konde Gang Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize.

 

Wawili hao waliachana Desemba mwaka jana na sasa Kajala ameonekana kufurahia hali yake ya pekee.
Jana Jumatano, mama ya mtoto mmoja (binti), alidokeza kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwamba alipitia shida nyingi katika uhusiano wake wa zamani.

 

Alifanya hivyo kwa kupost video yake akicheza na kuimba wimbo mpya wa Alikiba ‘Mahaba’ unaozungumzia masaibu yanayohusishwa na mahusiano yenye sumu.

“Uchungu wakulia kila siku
Mapenzi yalinifanya nisile
Sina kumbukumbu hile kwamba ulinikosha noo!
Uchungu wakulia daily
Mapenzi yalinifanya nisile
Sina kumbukumbu hile kwamba ulinitosha noo!
Mwenzako mi nilikufa nikazikwa nikaoza
Mapenzi yalinitesa yalinitupa nimefufuka yeh!
Mi nilikufa nikazikwa nikaoza
Mapenzi yalinitesa nimefufuka yeeh,” aliimba.

 

 

Wiki chache zilizopita mpenzi wa zamani wa Harmonize alidokeza kuwa yuko tayari kujitosa katika mahusiano mapya.
Mama ya mtoto mmoja aliweka wazi kuwa sasa yuko tayari kujaribu uhusiano na mtu wa ishara sawa ya zodiac naye, akimaanisha mtu anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa karibu wakati sawa na yeye.

 

“Nataka kuchumbiana na ishara yangu. Ninataka kuona ikiwa tuna tabia sawa na ikiwa tunadumu,” alisema kwenye Instagram.
Wakati akitangaza kuachana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana, Kajala aliweka wazi kuwa yuko tayari kupiga hatua nyingine baada ya uhusiano wao wa miezi michache kugonga mwamba.
Ingawa hakufichua kilichowatenganisha, aliweka wazi kuwa hakuwa na kinyongo chochote dhidi ya mwimbaji huyo.
“Mimi kama mwanamke na binadamu niliumbwa kupenda na kusamehe pia, lakini katika hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia.

 

Sipo hapa kwa ajili ya kujitetea au kujionea huruma, ni kweli nilifanya makosa na nimetambua makosa yangu, sijakamilika,” Kajala alisema Desemba.

 

Wanandoa hao wa zamani walikuwa wamechumbiana kwa takriban miezi saba kabla ya kutengana mapema Desemba. Wawili hao walikuwa wamerudiana mwezi Aprili baada ya Harmonize kuomba msamaha.
Wakati wa uhusiano wao, wawili hao walionekana kuwa na muungano mzuri na walifurahia kuwa pamoja.
Juni, walidokeza mpango wa kufunga ndoa baada ya Harmonize kumchumbia Kajala.

About The Author

1 thought on “Frida Kajala Azungumzia Mahusiano Na Harmonize Baada Ya Kutemana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!