Home » Mwanaume Amnajisi Mtoto Wa Miaka 9

Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi msichana wa miaka 9.

 

Akiwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa Martin Rabera, mshtakiwa alipatikana na hatia baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa mlalamishi.

 

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) leo hii Jumatano, imesema kuwa uamuzi huo ulipata ushahidi wa mlalamishi kuwa wa kutosha kuhukumiwa.

 

Mahakama pia imesema kuwa mtoto huyo bado ana kiwewe na anaendelea na ushauri nasaha na hivyo mshtakiwa hastahili adhabu ya kutokuwa rumande.

 

Mahakama imesema kuwa mshtakiwa hastahili hukumu isiyo ya kifungo.

 

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Barbara Sombo ulipinga ombi la upande wa utetezi la kutoa adhabu isiyokuwa ya rumande, kutokana na majeraha ya kimwili na kisaikolojia aliyoyapata mtoto huyo.

 

ODPP amesema mahakama iliona ni muhimu kutoa adhabu kali ili kuwadhibiti wahalifu wa kingono kutokana na kufanya uhalifu sawa na huo siku zijazo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!