Home » Alex Mwakideu Amkashifu Diana Marua

Mtangazaji wa redio Alex Mwakideu, amemkashifu mwimbaji Diana Marua kwa kumburuza mwanamke mwingine kwenye ugomvi wake wa mtandaoni na Andrew Kibe.

 

Mwakideu alisema Diana ametoka kwenye mwelekeo dhabiti alipoamua kumhusisha mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa zamani wa Andrew Kibe, kwenye vita vyao mtandaoni.

 

Marua alikuwa ameweka mitandaoni picha ya Kibe na mwanamke huyo, akimtaka amrudishe ikiwa yeye ndiye aliyemuumiza mtangazaji huyo wa zamani wa redio.

 

“Ikiwa mwanamke huyu katika picha hii ndiye aliyemvunja moyo mtangazaji huyu wa zamani wa redio, tunamwomba amrudie kwa sababu sisi wengine tunaumia juu ya talaka hii. Inakuwaje Kifee anachukia watu wote waliooana?” Marua alinukuu picha aliyoweka.

 

Lakini Mwakideu anasema ni makosa kumshirikisha mwanamke mwingine ambaye anaweza kuishi maisha yake kimya kimya, kulea watoto wake bila kusababisha drama.

 

Marua ambaye ameolewa na mwimbaji Bahati, amekuwa akizozana mara kwa mara na Kibe kwenye mitandao ya kijamii, huku wawili hao wakitoleana maneno.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!