Mashirika Yasiyo Ya serekali Tanzania Yahimizwa Kulipa Kodi
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) umetoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuzingatia sheria na kanuni za nchi hiyo ikiwemo ulipaji wa kodi ya kila mwaka pamoja na uwasilishaji taarifa ya kila mwaka.
Hii itasaidia kuepuka kusimamishwa kufanya kazi au kufutiwa usajili.
Tamko hilo limekuja baada ya notisi kutolewa na msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania, Februari 23 mwaka huu, kuonyesha kuwa mashirika 2915 yapo hatarini kufutwa usajili kwa kushindwa kuwasilisha taarifa zao kwa miaka zaidi ya miwili na kushindwa kulipa ada ya mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Uchechemuzi wa THRDC, Nuru Maro, amesema mashirika hayo yanapaswa kufuata kanuni na kuepuka kusimamishwa kufanya kazi au kufutiwa usajili.
Pia, aliwataka wafadhili kuzingatia uwiano wa rasilimali wanazotoa kwa mashirika yote na kutokuwa na upendeleo kwa baadhi ya mashirika na kuwashauri mashirika hayo, kuomba ruzuku kwa makundi ili kuweza kupata ruzuku za kuendesha shughuli zao.
Kwa upande wake, Wakili wa THRDC, Paul Kisabo, ameeleza kuwa changamoto zinazokumba mashirika hayo ni pamoja na ukosefu wa fedha, kushindwa kutoa taarifa ya mwaka na kulipia ada ya mwaka.
Ameongeza kuwa idadi ya mashirika hayo yaliyo hatarini kufutiwa usajili inaweza kufikia jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali 7794, ikiwa ni pamoja na yale 4879 yaliyofutiwa usajili Januari 24 mwaka huu.
Hata hivyo, THRDC imetoa wito kwa mashirika hayo kuzingatia kanuni na sheria za nchi ili kuepuka hatua za kisheria dhidi yao.
THRDC inaendelea kutoa ushauri na msaada kwa mashirika yote ya haki za binadamu nchini Tanzania ili kuimarisha utendaji wao na kuhakikisha kuwa wanafanya