Home » ‘Hakuna Uamuzi Wowote Ambao Umefanywa Wa Kuongeza Karo Za Vyuo Vikuu’ – Waziri Machogu

‘Hakuna Uamuzi Wowote Ambao Umefanywa Wa Kuongeza Karo Za Vyuo Vikuu’ – Waziri Machogu

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amevunja ukimya wake kuhusu madai ya mipango ya serikali kuongeza karo za vyuo vikuu kote nchini.

 

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya, Waziri Machogu amekiri kwamba pendekezo la kupandisha karo za chuo kikuu lilitolewa kwa Serikali lakini akasisitiza kuwa hakuna uamuzi wowote ambao umetolewa kuhusu suala hilo.

 

Kumekuwa na ripoti kwamba jopokazi lililoteuliwa na Rais William Ruto mwaka jana lilipendekeza nyongeza ya karo zinazolipwa katika vyuo vya elimu ya juu kama njia ya kusaidia taasisi hizo kuimarika kifedha.

 

Kulingana na ripoti hizo, serikali inanuia kulipa ada tatu za chuo kikuu kutoka kiwango cha sasa cha shilingi elfu 16, 000 kwa muhula hadi shilingi elfu 48, 000.

 

Wakati uo huo, Machogu amekanusha madai kwamba kuna mipango ya kubinafsisha vyuo vikuu vya umma nchini.

 

Machogu ameshikilia kuwa serikali imejitolea kusaidia sekta ndogo ya chuo kikuu kufikia malengo yake.

 

Kadhalika Amesema serikali itaendelea kuvisaidia vyuo vikuu vya umma kwa kuweka mazingira salama na kuthibitisha ufadhili kupitia mafunzo na mikopo kwa wanafunzi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!