Home » Mshukiwa Mkuu Wa Mauaji Ya Ivy Wangeci Ajitetea Katika Mahakama Ya Eldoret

Mshukiwa Mkuu Wa Mauaji Ya Ivy Wangeci Ajitetea Katika Mahakama Ya Eldoret

Naftali Kinuthia, mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanafunzi wa Udaktari wa Chuo Kikuu cha Moi Ivy Wangeci miaka mitatu iliyopita amefikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya mauaji.

 

Kinuthia alishtakiwa kwa kumkatakata Wangeci mara mbili kichwani kwa kutumia shoka nje ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH).

 

Alipokuwa mbele ya mahakama Machi 3, 2023, Kinuthia ameambia mahakama hiyo kwamba uhusiano wao ulianza tangu zamani kama marafiki wa utotoni ambao walikuwa majirani wa karibu.

 

Mshtakiwa pia amesimulia kwamba Ivy alimpigia simu kabla ya siku yake ya kuzaliwa akimjulisha kuwa sherehe yake ya kuzaliwa ingegharimu shilingi elfu 28,000, ambapo alimtumia shilingi elfu 14,000 kuanzisha hafla hiyo na kuahidi kumpelekea pesa zilizosalia yeye binafsi.

 

Kinuthia amesimulia kuwa juhudi zake za kutaka Wangeci azungumzie maswala yao ya kimapenzi ziliambulia patupu baada ya kumtembelea, na kudai kuwa marehemu alimjulisha kuwa alikuwa na shughuli nyingi na marafiki zake baada ya sherehe hiyo jambo lililomghadhabisha.

 

Akiwa amechanganyikiwa kutokana na kupoteza uhusiano aliokuwa nao na marehemu, Kinuthia anadai kuwa alienda kwenye gari lake na kuchukua shoka ambalo alitumia kumshambulia marehemu.

 

Kulingana na Kinuthia amesimulia kwamba fahamu ilirudi alipokuwa hospitalini baada ya kundi la watu kumvamia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!