Home » Johnson Muthama Aapishwa Kama Kamishna wa Huduma Za Bunge

Johnson Muthama Aapishwa Kama Kamishna wa Huduma Za Bunge

Seneta wa Machakos Johnson Muthama ameapishwa kuwa mmoja wa Makamishna wa Tume ya Huduma za Bunge (PSC).

 

Muthama amechukua wadhifa huo baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa na Seneti kufuatia uteuzi wake na kuchujwa kwa mahojiano yaliyofanywa Desemba mwaka jana.

 

Hafla ya kuapishwa ilifanyika jana katika majengo ya Bunge na kuongozwa na Spika wa Bunge Moses Wetangula ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge akihudhuriwa na makamishna wengine.

 

Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni pamoja na; Seneta Mteule Joyce Korir ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Seneta wa Nyamira Okongo Omogeni, Seneta wa Laikipia John Kinyua, Mbunge wa Likoni Mishi Mboko, Mbunge wa Kaunti ya Nyandarua Faith Gitau.

 

Makamishna wengine wa Utumishi wa Bunge ni; Mbunge wa Nyali Mohamed Ali, Mbunge wa Mavoko Patrick Makau, Aliyekuwa Mbunge wa Kaunti ya Kakamega Rachel Ameso na Karani wa Seneti Jeremiah Nyegenye ambaye ni Katibu wa Tume hiyo.

 

 

Alitoa wito kwa Tume ya Utumishi wa Bunge kusaidia kutatua kwa amani tofauti kati ya Bunge la Kitaifa na Seneti kwa kuwa zote ni mabunge yenye jukumu kuu la kuwakilisha masilahi ya raia.

 

Wetangula aliitaka tume hiyo iliyoundwa kikamilifu kufanya kazi bila kuegemea upande wowote kwa kuwa sasa wamepewa jukumu la kutumikia maslahi ya Wabunge wote 416 ambao ni wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa na hawapaswi kujikita katika misimamo yao ya kisiasa.

 

Muthama alisema kuwa amehudumu kama Mbunge na Seneta kwa miaka mingi kunamweka katika nafasi nzuri ya kuhudumu kama Mwanachama wa Tume ya Utumishi wa Bunge akiwahakikishia Wabunge kuwa atasimamia maslahi yao kila wakati.

 

Aidha, Muthama alisema kuwa uzoefu wake kama Mbunge ambapo wakati fulani aliwahi kuwa mnadhimu mkuu ulimtayarisha ya kutosha kwa kazi ya kuwa Kamishna katika Tume ya Utumishi wa Bunge.

 

Seneta huyo wa zamani wa Machakos aliambia kamati hiyo kuwa ameongoza zoezi la uteuzi huru na wa haki katika chama tawala hali iliyopelekea kufanya vyema katika uchaguzi mkuu wa hivi majuzi ikilinganishwa na vyama vingine na atahakikisha kuwa tume hiyo inasimamia ustawi wa wanachama wote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!