Home » Wasiwasi Waibuka Baada Ya Asilimia 33 Pekee Ya Wasichana Nchini Kenya Kujitokeza Kupata Chanjo Ya HPV

Wasiwasi Waibuka Baada Ya Asilimia 33 Pekee Ya Wasichana Nchini Kenya Kujitokeza Kupata Chanjo Ya HPV

Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa wito wa matumizi zaidi ya chanjo ya Human Papillomavirus (HPV), kwani ni asilimia 33 tu ya wasichana nchini Kenya wamechanjwa.

 

Kulingana na Wizara ya Afya, asilimia 61 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 10 na 14 wamepata dozi ya kwanza ya chanjo, na asilimia 31 walipata dozi ya pili.

 

Dk.Mary Nyangasi, Mkuu wa Mpango wa Kitaifa wa Saratani anasema idadi kubwa ya wanawake walioathiriwa na saratani wanatoka katika familia maskini wanaoishi vijijini na pia wana kiwango cha chini cha elimu.

 

Amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wa kike kupata chanjo ya HPV, ikiwa ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.

 

Wizara ya afya inabainisha kuwa takwimu zinaonyesha wanawake 9 hufariki kutokana na saratani ya shingo ya kizazi nchini Kenya kila siku, na hilo linaweza kuzuiwa kwa chanjo.

 

Aidha Inalenga kufikia asilimia 90 ya chanjo kamili ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.

 

Nyangasi anaongeza kuwa asilimia 50 ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi nchini Kenya hugundulika katika hatua za awali ambapo wagonjwa asilimia 90 wanapata matibabu.

 

Gavana wa Embu Cecily Mbarire ameahidi kushinikiza mpango wa saratani katika Baraza la Magavana, na kuwataka wakuu wa kaunti kuzingatia mikakati ya kuzuia ugonjwa huo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!