Home » Waangalizi Wa Umoja Wa Ulaya Wakosoa Kushindwa Kwa Uwazi Katika Uchaguzi Wa Nigeria

Waangalizi Wa Umoja Wa Ulaya Wakosoa Kushindwa Kwa Uwazi Katika Uchaguzi Wa Nigeria

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umekosoa ukosefu wa uwazi na kushindwa kwa utendaji katika uchaguzi wa Nigeria, kulingana na matokeo yake ya awali.

 

Umoja huo umesema kuna imani katika uhuru na weledi wa chombo cha uchaguzi wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.

 

Lakini imani ya umma ilipungua kutokana na kukosekana kwa mipango madhubuti na mawasiliano katika mchakato huo ikiwa ni pamoja na siku ya uchaguzi.

 

Raia wa Nigeria walipiga kura zao katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge siku ya Jumamosi.

 

Waangalizi hao wamebaini kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilichelewa kufunguliwa na taratibu za upigaji kura hazikufuatwa kila mara.

Aidha Wamesema upakiaji wa matokeo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki haukufaulu, hivyo kuzua wasiwasi kwani uwasilishaji wa fomu za matokeo ya uchaguzi wa urais ulicheleweshwa.

 

Timu ya waangalizi hao imewataka wadau katika uchaguzi huo kusimamia amani hadi mchakato huo utakapokamilika na kutaka migogoro itakayojitokeza ishughulikiwe kwa njia za kisheria.

Ikumbukwe Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta yuko nchini Nigeria ambako amehusika na uchunguzi wa uchaguzi uliokamilika jumamosi.

 

Rais mstaafu amewataka raia wa Nigeria kuwa na utulivu hata wanaposubiri matokeo ya urais Uchaguzi wa taifa hilo ulifanyika kwa njia ya amani, raia wa taifa hilo wanatafuta mrithi wa Rais Muhammadu Buhari anayestaafu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!