Home » Kenya Yapata Msaada Wa Shilingi Billioni 16 Kutoka Kwa Serikali Ya Marekani

Kenya Yapata Msaada Wa Shilingi Billioni 16 Kutoka Kwa Serikali Ya Marekani

President Joe Biden and First Lady Jill Biden pose for photo line photos with President William Ruto and his wife Rachel during the U.S.-Africa Leader Summit, Wednesday, December 14, 2022, in the Diplomatic Reception Room of the White House. Photo|PCS

Serikali ya Marekani imetoa angalau shilingi bilioni 16 kuunga mkono juhudi za Kenya za kukabiliana na ukame.

 

Kulingana na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), fedha hizo zitasaidia kukidhi mahitaji ya dharura kwa takriban watu milioni 1.3 kote nchini Kenya.

 

Msaada wa ziada wa chakula kwa Kenya unakuja huku kukiwa na ukame unaoendelea ambao umewaacha zaidi ya watu milioni nne katika hali mbaya ya njaa, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka hadi zaidi ya milioni tano ifikapo Juni mwaka huu.

 

Baada ya msimu wa tano wa mvua kukatika katika Pembe ya Afrika, mvua nyingi nchini Kenya sasa ni chini ya asilimia 70 ya wastani wa miaka 30 kote nchini na kuzidisha mahitaji ya kibinadamu.

 

USAID itatoa chakula cha dharura kama vile mtama, mahindi, mbaazi, na mafuta ya mboga kwa familia zinazoishi katika maeneo ambayo masoko ya ndani hayapatikani.

 

Zaidi ya hayo, katika maeneo ambayo masoko yanafanya kazi, washirika watatoa usaidizi wa pesa taslimu kwa familia.
Aidha msaada huo pia utasaidia mipango ya kuzuia na kutibu utapiamlo kwa watoto, kwani zaidi ya watoto elfu mia 970,000 wenye umri wa miaka mitano na chini wana utapiamlo wa hali ya juu nchini kote.

 

Rais William Ruto amekaribisha tangazo hilo ambalo linakuja kufuatia ziara ya mke wa Rais wa Marekani Jill Biden nchini.

 

Akitumia Twitter, rais ameelezea shukrani zake kwa msaada huo huku nchi ikikumbwa na ukame mbaya zaidi kutokana na miaka 4 ya mvua iliyofeli.

 

“Kwa niaba ya watu wa Kenya, shukrani zangu za dhati ni kwa serikali ya Marekani kwa msaada huu wa ukarimu kwa watu wanaostahili sana wanaokabiliwa na ukame mbaya zaidi kutokana na mvua zilizokatika kwa miaka 4 mfululizo., ” alisema Rais Ruto.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!