Home » Mwili Wa Mwanamume Aliyeripotiwa Kutoweka Wapatikana Katika Yyumba Yake Jijini Nairobi

Polisi jijini Nairobi wanachunguza kifo cha mwanamume wa makamo aliyepatikana amefariki katika nyumba yake kando ya barabara ya Mbagathi, eneo bunge la Lang’ata.

 

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu, aliyetambuliwa kama Martin Nyaga huenda alijiua.

 

Afisa mkuu wa polisi kaunti ndogo ya Lang’ata Monica Kimani amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa mwili wa marehemu ambaye alikuwa ameripotiwa kutoweka kwa siku kadhaa tayari umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

 

Polisi ambao wametahadharishwa na mlinzi wa ghorofa hiyo, walilazimika kuingia ndani ya nyumba hiyo na kukuta mwili huo ukining’inia kwenye dari huku akiwa amefungwa kamba shingoni.

 

Kwingineko katika Kaunti ya Mombasa, polisi wanawasaka majambazi wawili waliojihami walioiba kiasi kisichojulikana cha pesa na vifaa vya simu kutoka kwa duka la M-Pesa eneo la Bamburi.

 

Kulingana na kanda ya CCTV iliyoshirikiwa na polisi, mmoja wa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi anaonekana akiingia kwenye duka la M-Pesa na kutoa bunduki aina ya AK-47 kwenye mkoba wake huku mshirika wake akipora droo za kukusanya pesa na vifaa vingine vya rununu.

 

Hata hivyo, mwanamke aliyekuwa katika duka hilo aliachwa bila madhara wakati wa tukio la Jumapili, Februari 26.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!