Home » Waziri Wa Mazingira Ataka Huduma Za Hali Ya Hewa Zitathminiwe

Kuna haja ya kuboresha Huduma za Hali ya Hewa nchini Kenya ili kuwapa raia taarifa za uhakika za hali ya hewa kwa tahadhari ya mapema na kufanya maamuzi ndio kauli yake Waziri wa Mazingira na misitu Soipan Tuya.

 

Waizir Tuya amebainisha kuwa Wizara yake itafanya Marejesho ya Mfumo wa Ikolojia unaojumuisha Kampeni ya Kitaifa ya Ukuzaji na Urejeshaji wa Miti Bilioni 15 kote nchini ili kuongeza miti kutoka asilimia 12 hadi 30 ifikapo 2032.

 

Waziri wa Mazingira, Soipan Tuya alikuwa akizungumza katika Kamati ya Kitaifa ya Idara ya Mazingira, Misitu na Madini ya Bunge kwa kuzingatia Sera ya Bajeti ya 2023 .

 

Alisema mambo yanayoweza kutekelezwa na Wizara ni pamoja na Kukabiliana na Mabadiliko ya, Usimamizi wa Taka Endelevu na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa mzunguko, kusaidia maisha na kuongeza ajira, kuboresha huduma za Hali ya Hewa.

 

Kulingana naye, 2023/24 Wizara ya Mazingira imetengewa bajeti ya Maendeleo ya Ksh Bilioni 4.988 dhidi ya mahitaji ya bajeti ya Ksh bilioni 13.269 hii ikiwakilisha asilimia 40 ya mahitaji yote.

 

Mkutano huo ambao uliongozwa na David Gikaria (Mji wa Nakuru Magharibi) na Naibu Charles Kamuren (Baringo Kusini) unakusudiwa kujadili sera kuu za kisekta zinazozingatia ukomo wa matumizi, programu muhimu, matokeo na shabaha katika muda wa Kati miongoni mwa mengine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!