Serikali Ya Kenya Kwanza Kushughulikia Wakenya Wote Asema Rais Ruto
Rais William Ruto amesema kuwa utawala wake hautakuwa na upendeleo katika kutoa huduma kwa Wakenya wote bila kujali waliompigia kura wakati wa uchaguzi wa Agosti 2022.
Akizungumza wakati wa ibada ya shukrani huko Lamu Jumapili, Rais Ruto alisema kuwa serikali yake inalenga kutimiza ahadi zake wakati wa kampeni na kwamba Wakenya wote watafaidika na ajenda zake ya maendeleo.
Aidha, Mkuu huyo wa Nchi amewataka Wakenya kuishi kwa utangamano, akisema kuwa maendeleo yatafaa iwapo taifa litaungana na kufuata mkondo huo.
Sambamba na hilo, Rais Ruto amesema kuwa ni kinyume na msingi wa ahadi zake ya kushughulikia mizozo ya kudumu ya ardhi inayoshuhudiwa Lamu na kudai kuwa atahakikisha kila mhusika anapata vibali vyao halali.
Rais Ruto aliandamana na Naibu wake Rigathi Gachagua, Waziri Mkuu Musalia Mudavadi, gavana wa Lamu Issa Timamy pamoja na viongozi wengine serikalini.
Naye Naibu Rais Rigathi Gachagua amewasuta viongozi waliokuwepo wakati wa serikal iliyopita kwa kuchangia kuzorota kwa uchumi wa taifa.