Serikali Yafafanua Kuhusu Uhaba wa Umeme
Kampuni ya Kuzalisha Umeme nchini (KenGen) imekashifu madai ya uhaba wa umeme nchini kutokana na mvua ndogo inayotarajiwa nchini.
Akizungumza mjini Olkaria, Mkurugenzi Mtendaji Abraham Serem ameshikilia kuwa viwango vya chini havitaathiri uzalishaji wa nguvu za umeme.
Serem amefichua kuwa serikali ilikuwa ikiagiza umeme kutoka Ethiopia ili kukidhi nakisi katika uzalishaji wa umeme.
Serem amebainisha kuwa KenGen ilianza kugawa matumizi ya umeme unaozalishwa kwa kutumia maji na iliutumia tu wakati mahitaji yalikuwa makubwa.
Wakati uo huo, Kenya inaendelea kufanya kazi na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) ili kuharakisha uzalishaji wa nishati huku ikipunguza kasi ya kutegemea umeme wa joto.
Ufafanuzi huo ulijiri siku chache baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Kiuchumi la Rais William Ruto David Ndii kuwaambia Wakenya kwamba serikali inalenga kuzalisha nguvu za kutegemewa na si za bei nafuu.