Home » Raila Acheka Kushinikiza Marufuku Ya Kusafiri, Asema “Ni Utoto”

Raila Acheka Kushinikiza Marufuku Ya Kusafiri, Asema “Ni Utoto”

Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga anasema haogopi kupigwa marufuku kuzuru nchi yoyote ng’ambo kama wanakubaliana na ukweli kwamba matatizo ya Kenya lazima yatatuliwe na Wakenya wenyewe.

 

Raila Anasema wito unaodaiwa na Kenya Kwanza kwenda Magharibi na nchi washirika kumpiga marufuku kutembelea nchi zao ni hali yakuonyesha jinsi wanavyoashiria kushindwa na vitendo vya uoga.

 

Akizungumza katika mji wa Kitale Odinga ameonya dhidi ya hatua zozote za kushinikiza marufuku ya kusafiri akisema ni kinyume cha sheria.
Kiongozi wa upinzani ambaye anasisitiza kuwa alishinda uchaguzi wa rais wa Agosti 2022 ameambia nchi za Magharibi kupuuza wito kama huo.

 

Aidha ametetea msukumo wake wa kuchukuliwa hatua kwa wingi akisema unalenga kuzuia dhuluma katika uchaguzi na kuhakikisha matakwa ya watu yanaheshimiwa.

 

Kulingana na Raila hatarudi nyuma hadi ushindi wake unaodaiwa urejeshwe kwake.

 

Rais William Ruto wiki jana, alikejeli matakwa ya Upinzani akisema sava zilifunguliwa Wakenya walipoenda vituoni na kutambuliwa kibayometriki kabla ya kupiga kura zao.

 

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ilimtangaza Rais Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi uliopita baada ya kupata kura milioni 7,176,141, sawa na asilimia 50.59 ya kura halali zilizopigwa ikilinganishwa na milioni 6,942,930 za Raila akiwakilisha asilimia 48.85…raila ametumia fursa hiyo kuwashinikiza wakazi wa kaunti ya Trans nzoia ambako aliongoza mkutano kutokubali uongozi wa Kenya kwanza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!