Home » Wizara Ya Leba Yaanzisha Uchunguzi Kuhusu Unyanyasaji Wa Kingono Katika Mashamba Ya Chai

Wizara Ya Leba Yaanzisha Uchunguzi Kuhusu Unyanyasaji Wa Kingono Katika Mashamba Ya Chai

Wizara ya leba imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake wa kazi katika mashamba mawili ya majani-chai yanayomilikiwa na makampuni ya Uingereza nchini Kenya.

 

Katika taarifa ya leo hii Katibu Mkuu katika Idara ya Kazi ya Serikali Geoffrey Kaituko anasema serikali inachukulia madai hayo kwa uzito huku akionyesha wasiwasi kwamba vitendo kama hivyo vinaweza kutokea.

 

Kaituko amefichua kuwa Wizara inashirikisha pande zote zinazohusika ikiwa ni pamoja na wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata undani wa suala hilo.

 

Kulingana na naye, matokeo ya uchunguzi yatatolewa kwa umma mara tu itakapokamilika na kusema ufichuzi wa hivi punde unaonyesha mazingira ya uhasama katika kampuni hizo mbili, ambayo hayafai kuachwa hata kama alikariri kuwa unyanyasaji wa kijinsia ni kosa la jinai.

 

Ufichuzi wa unyanyasaji wa kingono katika makampuni hayo mawili ulidhihirika mapema wiki hii katika makala ya uchunguzi iliyopeperushwa na BBC.

 

Katika filamu hiyo, shirika la utangazaji la Uingereza linasema liligundua zaidi ya wanawake 70 wamenyanyaswa na wasimamizi wao kwenye mashamba yaliyoendeshwa, kwa miaka mingi, na Unilever na James Finlay.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!