Serikali Kununua Mahindi Kutoka Kwa Wakulima Kwa Shilingi 5,600
Ni afueni kwa wakulima kwani Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) imetangaza kuwa wameongeza bei ya kununua mahindi kutoka kwa wakulima wa humu nchini.
Akiwa mbele ya Kamati ya Utawala na Kilimo ya, Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo Joseph Kimeto amesema kuwa wamerekebisha bei kutoka Shilingi elfu 5,100 hadi Shilingi elfu 5,600 kwa mfuko wa kilo 90.
Wakulima walikuwa wamelalamika kwamba wana hatari ya kupata hasara kwani serikali ilikuwa imetangaza kuwa itafungua dirisha lisilotozwa ushuru kwa uagizaji wa mahindi ili kupunguza pengo hilo.
Kufikia sasa, NCPB imehifadhi mifuko 50,000 kwa madhumuni ya kibiashara.
Aidha, Kimeto amewaambia wabunge kuwa mchakato wa kuuza mafuta kwa ruzuku unaendelea katika kaunti 12.
Serikali inanuia kusambaza magunia milioni 6 kabla ya mwisho wa msimu wa upanzi katika eneo la kaskazini na kusini mwa bonde la ufa vile vile eno la Nyanza.