Thamani yangu Ni Milioni 250, Asema Mwanasheria Mkuu Aliyeteuliwa Shadrack Mose
Mgombea wa nafasi ya Wakili Mkuu Shadrack John Mose anasema thamani yake ya kifedha ni Ksh milioni 250.
Ametoa madai hayo leo hii Alhamisi asubuhi alipokuwa mbele ya Kamati ya Kitaifa ya Idara ya Haki na Masuala ya Kisheria (JLAC) kuchunguzwa ili kujaza nafasi hiyo.
Mose alisema mapato hayo yanatokana na kodi, ardhi, na hisa za kampuni yake ya uwakili.
Akielezea vipaumbele vyake mara tu atakapoidhinishwa, Mose alisema juu katika orodha yake ni kuhakikisha wafanyikazi katika ofisi ya sheria ya serikali wanahesabiwa upya kulingana na mzigo mkubwa wa kazi.
Aidha alieleza kusikitishwa na kujiuzulu kwa Mawakili wa Serikali ambao alihusisha na mazingira duni ya kazi, hali inayoendelea kuzorotesha utoaji wa huduma na utoaji haki.
Mose pia alianzisha mafunzo makali kwa maafisa hao ili kuongeza uwezo wao wa kushughulikia masuala tata ya kisheria.
JLAC inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake mnamo au kabla ya Alhamisi, Machi 9, 2023, ili kuwezesha Bunge kuzingatia suala hilo ndani ya muda uliowekwa kisheria.
Mbunge huyo wa zamani wa Kitutu Masaba ana Stashahada ya Uzamili ya Sheria, kutoka Shule ya Sheria ya Kenya, pamoja na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Yeye ni wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya mwenye tajriba ya zaidi ya miaka 29 katika utendaji wa sheria.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu sifa za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kamati inatarajia mteule huyo kuonyesha ujuzi mkubwa wa sheria na uelewa wa mazingira anayotarajiwa kuhudumu.
Iwapo ataidhinishwa, Shadrack Mose atachukua nafasi ya Kennedy Ogeto ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo Machi 2018.
Hii inafuatia kuteuliwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Kitutu Masaba na Rais William Ruto mnamo Februari 13, 2023.