Home » Aisha Jumwa: Mtumishi Wa Umma Ambaye Ametimiza Umri Wa Kustaafu Anapaswa Kuondoka Ofisini

Aisha Jumwa: Mtumishi Wa Umma Ambaye Ametimiza Umri Wa Kustaafu Anapaswa Kuondoka Ofisini

Waziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia, Aisha Jumwa amesema yuko kwenye dhamira ya kuwaondoa watumishi wa umma ambao bado wako madarakani licha ya kufikisha umri wa kustaafu.

 

Katika mahojiano na runinga moja humu nchini, Jumwa amesema tangu achukue wadhifa wake, amegundua kuwa afisi nyingi za mashirika ya umma zimejaa wafanyikazi ambao wametimiza umri wa kustaafu na wanapaswa kurudishwa nyumbani.

 

Jumwa ameongeza kuwa imekuwa desturi kwamba watu ambao wamepita pengo la umri wa kustaafu kuongezwa kandarasi ilhali vijana wanakabiliana na uhaba wa nafasi za kazi.

 

Kulingana na Jumwa, tayari ameiandikia Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) kuhoji suala hilo na kumtimua yeyote ambaye amepita kizingiti cha umri.

 

Waziri wa Utumishi wa Umma ameendelea kuongeza kuwa pendekezo lake litafungua njia kwa ajili ya mpito usio na mshono kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika sekta ya kazi.

 

Sheria ya PSC, 2017 inasema kwamba umri wa lazima wa kustaafu katika utumishi wa umma utakuwa miaka sitini na miaka sitini na mitano kwa watu wenye ulemavu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!