Home » Sapit Ajiunga Na Uasi Wa Kanisa La Anglikana juu ya ndoa za mashoga

Kanisa la Anglikana Kenya (ACK) lImejiunga na watu mbalimbali kupinga madaio dhidi ya kanisa Wingereza , kuhusu uamuzi wake wa kubariki ndoa za mashoga.

 

Mkuu wa ACK, Askofu Mkuu Jackson Ole Sapit ameonya kwamba ushirika wa Kianglikana nchini Kenya hautawahi kutambua wala kubariki ndoa za watu wa jinsia moja kwani zinakiuka mafundisho ya Biblia.

 

Sapit ameungana na viongozi wengine 12 wa kanisa la Anglikana ambao wametangaza kwamba hawamfikirii tena Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, kuwa kiongozi wa ushirika wa kimataifa kufuatia uamuzi wake wa kuruhusu baraka kwa ushirikiano wa mashoga.

 

Viongozi, ambao wanasema wanawakilisha asilimia 75 ya Waanglikana duniani kote wameshutumu Kanisa la Uingereza kwa kuchukua “njia ya mafundisho ya uongo”, na kwenda kinyume na “imani ya kihistoria ya Biblia.”

 

Wamemshutumu Askofu Mkuu Welby ambaye aliongoza Baraza la Maaskofu wake kutoa mapendekezo ya kuwabariki wanandoa wa jinsia moja wakijua kwamba wanaenda kinyume na imani na utaratibu wa majimbo ya kiorthodox katika ushirika’.

 

Waliotia saini ni pamoja na mwenyekiti wa GSFA, Askofu Mkuu Justin Badi, pamoja na maaskofu wakuu wa Chile, Bahari ya Hindi, Kongo, Myanmar, Bangladesh, Uganda, Sudan, Alexandria na Melanesia.

 

Tangu ilipoanzishwa mwaka wa 1867, Askofu Mkuu aliye madarakani wa Canterbury amechukua nafasi ya kiongozi wa kiroho wa Ushirika wa Kianglikana, ushirika wa kimataifa wa makanisa 42 ya Kianglikana. Kati ya majimbo 25 wanachama wa GSFA, 22 ni sehemu ya Ushirika mpana wa Anglikana.

 

Msemaji wa ikulu alisema Askofu Mkuu anawasiliana mara kwa mara na Wazee wenzake na anatazamia kujadiliana nao mambo hayo na mengine katika kipindi kijacho.

About The Author

1 thought on “Sapit Ajiunga Na Uasi Wa Kanisa La Anglikana juu ya ndoa za mashoga

  1. Relativity of sin. It is interesting how LQBTQ associated with individual orientation or peversion which does not affect others directly is more sin than the sin of corruption, which directly leads to deaths. The church is corrupt! This must be condemned more!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!