Home » Viongozi Wa Dini, Serikali Waungana Kukemea Ushoga Na Usagaji
Viongozi wa dini nchini Tanzania wameipongeza serikali ya nchi hiyo baada ya kupiga marufuku vitabu 16 kutumika katika shule za msingi na sekondari ambavyo vinadhaniwa kuwa vinahamasisha mapenzi ya jinsia moja, kitendo ambacho kimekemewa vikali na jamii kutokana na kuwa ni kinyume ya maadili ya jamii ya nchi hiyo pamoja na mila na desturi za Watanzania.
Akizungumza baada ya ibada ya swala ya Ijumaa leo imamu mkuu wa msikiti wa Mwinyimkuu uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania  Sheikh Juma Kijepa amempongeza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwa kuchukua hatua hiyo ya kupiga marufuku vitabu hivyo.
“Sisi viongozi wa dini kazi yetu kubwa ni kuwajenga waumini wetu katika maadili mema hivyo kitendo cha Wizara ya Elimu kupiga marufuku vitabu hivyo inatupa imani sisi viongozi wa dini kwa kuona kuwa serikali inatusikia na inaungana na sisi katika kukemea vitendo viovu”.
Kiongozi huyo ametilia mkazo agizo la Waziri huyo kwa Wazazi kuwa makini na watoto wao kwa kufanya ukaguzo wa mara kwa mara katika mabegi yao ili kudhibiti watoto wao kuendelea kuvitumia vitabu hivyo.
“Viongozi wa dini tumepiga kelele kuhusu mmomonyoko wa maadili hasa dhidi ya vitendo hivyo vibaya lakini hatujaona mapokeo na maoni  ya wazazi na walezi kuungana na serikali hapa nchini katika kupinga vitendo hivyo vibaya, tunawaomba wazazi na walezi kuwa makini na watoto wetu kwani dunia ya sasa inakabiliwa na hatari ikiwemo utandawazi”, Alisema Kijepa.
Hata hivyo Februari 13  mwaka huu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia wa nchi hiyo Prof. Adolf Mkenda katika mkutano wake na wanahabari jijini Dodoma alitangaza kupiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye Shule na Taasisi zote za Elimu kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 59 cha Sheria ya Elimu Sura ya 353.Ambapo alinukuliwa  akisema kama taifa tuna mila na desturi za  kufuata na katika kufundisha na kulea watoto na kwamba shule zina wajibu wa kuendana na taratibu hizo katika kuwaandaa watoto.
“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,”amesema Profesa MkendaAmevitaja vitabu
Februari 16 Pia Waziri Mkuu wa nchi hiyo Kasimu Majaliwa aliiagiza Sekta ya elimu nchini humo kufuatilia vitabu hivyo katika shule zote nchini zilizo za binafsi na shule za serikali lengo ni kudhibiti kuenea kwa vitabu hivyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!