Home » Tetemeko La Ardhi Tanzania
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 4.3 na 4.9 limeikumba mikoa ya Singida na Dodoma nchini Tanzania  leo Februari 17,2023 Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imethibitisha.
Katika taarifa ambayo imetolewa na GST, imesema haijapokea taarifa za madhara yoyote kufuatia tetemeko hilo ambalo limezua taharuki kubwa kwa wakazi wa mikoa hiyo na maeneo ya jirani.
“Ikumbukwe kwamba mikoa ya Singida na Dodoma nchini humo imepitiwa na Ukanda wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki mkondo wa Mashariki. Maeneo ya ukanda wa Bonde la Ufa kwa kawaida ni maeneo tete ya mabadiliko ya kijiolojia ambayo hukumbwa na matetemeko ya ardhi na milipuko ya volkano,” imesema taarifa hiyo.
Pia, Februari 9 mwaka huu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 4.7 lilitokea visiwani Pemba Tanzania visiwani yaani upande wa Zanzibar na kusikika katika baadhi ya miji nchi ya Tanzania na Kenya.
Vilevile ni wiki mbili zimepita tangu limetokea tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 nchini Uturuki, Siria ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha na kujeruhiwa na majengo na miundombinu kadhaa kuharibiwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!