Home » Ruto: Serikali Kuwajibika Kikamilifu Kwa Fedha Zinazotolewa Ili Kukabiliana Na Ukame

Ruto: Serikali Kuwajibika Kikamilifu Kwa Fedha Zinazotolewa Ili Kukabiliana Na Ukame

Rais William Ruto amesema kuwa utawala wake utatoa hesabu kamili ya fedha zilizochangwa ili kukabiliana na ukame unaozidi kuwa mbaya zaidi unaowakabili Wakenya.

 

Akizungumza baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Mvua za Muda Mfupi 2022 (Oktoba hadi Desemba) katika Ikulu ya Nairobi, Alhamisi, Rais amesema ukame huo mkubwa umesababisha dhiki na mateso mengi miongoni mwa Wakenya kutoka maeneo yaliyoathiriwa.

 

Akiwa ameambatana na Naibu wake, Makatibu wa Baraza la Mawaziri, Wanadiplomasia, Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya Kukabiliana na Ukame na sekta binafsi, Mkuu wa Nchi amewataka wadau wa maendeleo, sekta binafsi na watu wenye mapenzi mema kujitokeza na kuiunga mkono serikali katika kuokoa maisha ya watu na kujenga uvumilivu wa muda mrefu.

 

Ripoti ya Tathmini ya Mvua za Muda Mfupi 2022 (Oktoba hadi Desemba) iliyozinduliwa na Rais imeangazia kaunti 32 za ukame na zisizo za ukame.

 

Ripoti hiyo imebainisha athari za mvua hizo fupi kwa usalama wa chakula na lishe katika kaunti 32 zinazolengwa, kwa kuzingatia limbikizo la misimu ya mvua iliyopita na athari za majanga mengine yanayohusiana na usalama wa chakula na kupendekeza afua za kipaumbele.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!