Home » Ajali Ya Basi Na Lori La Kivita Yaua Watu 20 Nchini Afrika Kusini

Ajali Ya Basi Na Lori La Kivita Yaua Watu 20 Nchini Afrika Kusini

Ajali kati ya lori la kivita na basi imesababisha vifo vya watu 20 na wengine 60 kujeruhiwa katika jimbo la kaskazini mwa Afrika Kusini la Limpopo kulingana na idara ya usafiri nchini humo.

 

Kumi kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya na wamesafirishwa hadi hospitali.

 

Maafisa wa Polisi walikuwa wakipekua mto unaopita kando ya barabara kuu “kutafuta watu ambao huenda wamefagiliwa.”

 

Chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa, lakini mvua kubwa imekuwa ikinyesha eneo hilo katika siku za hivi karibuni, msemaji wa idara hiyo, Tidimalo Chuene, aliiambia AFP.

 

Mvua kubwa imesababisha mafuriko katika mikoa kadhaa ya Afrika Kusini katika siku za hivi karibuni, na kuua takriban watu saba na kupelekea serikali kutangaza janga la kitaifa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!