Home » Washukiwa 8 Wanaohusika Na Ulaghai Wa Ksh 500M Fuliza Wakamatwa Nakuru

Washukiwa 8 Wanaohusika Na Ulaghai Wa Ksh 500M Fuliza Wakamatwa Nakuru

Polisi mjini Nakuru wamewakamata washukiwa wanane wanaohusika na ulaghai wa shilingi milioni mia 500 za Fuliza.

Kulingana na polisi, kundi hilo la ngazi ya juu lilipatikana likiwa na nambari mpya 123,000 za simu za rununu zilizochaguliwa kuingia Fuliza mnamo Januari 2022.

 

Isaack Kipkemoi, Gideon Rono, Maxwell Ributhu, Gideon Kirui, Moses Rono, Collins Kipyegon na Edwin Cheruiyot, walikamatwa katika ghorofa moja huko Kiamunyi, huku Peter Gitahi akikamatwa Kitale, Kaunti ya Trans-Nzoia kufuatia oparesheni ya kina ya maafisa.

Maafisa wa polisi walianza uchunguzi kuhusu ulaghai huo uliopangwa baada ya ripoti kuwasilishwa kwa Kitengo cha Uchunguzi wa Ulaghai wa Kibenki (BFIU) mnamo Agosti 2022, baada ya wasimamizi wa hazina hiyo kugundua ongezeko lisilo la kawaida la upokeaji wa mkopo wa Fuliza ambao ulikuwa juu ya kiwango cha utendakazi wao na wakopaji walikuwa hawarejeshi mikopo.

 

Kulingana na BFIU, zaidi ya nambari mpya 123,000 za simu za rununu zilichaguliwa kutumia fuliza na kuchukua mikopo mnamo Januari 2022.

Zaidi ya hayo, wapelelezi walifichua kuwa baadhi ya laini hizo zilikuwa zimesajiliwa kama mawakala wa Safaricom ambapo pesa zilizokopwa zingewekwa kwenye akaunti za benki za watu hao.

Washukiwa hao, ambao wanaishi katika ghorofa kubwa huko Kiamunyi, kupitia ufundi wao wamenunua Subarus mbili mpya, Toyota Mark X moja, Toyota Probox, na pikipiki mbili kwa urahisi wa kusafiri.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!