Home » Mahakama Ya EAC Kusikiliza Kesi Ya Kuondolewa Kwa Sonko

Mahakama ya Afrika Mashariki imebuni jopo la majaji watano kusikiliza rufaa ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Juu dhidi yake.

 

Jopo la majaji watano linalojumuisha majaji Yohane Masara, Dkt.Charles Nyawello, Richard Muhumuza, Richard Wabwire Wejuli na Dkt. Gacuko Leonard, litasikiliza ombi lililowasilishwa na aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini Kenya kuhusu kuondolewa kwake madarakani ofisi.

Aidha, kikao cha kwanza kimepangwa kusikilizwa Jumatatu tarehe 27 Machi 2023 kuanzia saa 9.30 asubuhi mbele ya Jaji Yohane B. Masara Jaji Mkuu, Jaji Dk. Charles Nyawello, Jaji Richard Muhumuza, Jaji Mkuu Jaji Richard Wabwire Wejuli na Jaji Dk. Gacuko Leonard wakiwa katika Mahakama ya wazi, Ghorofa ya 2, Makao Makuu ya EAC, Barabara ya Afrika Mashariki EAC Close, Arusha

 

Haya yanajiri baada ya Gavana huyo wa zamani wa Nairobi kuhamia Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi wa kuidhinisha kuondolewa kwake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!