Mkewe Fundi Wa umeme Apigwa Na Umeme Hadi Kufa

Maafisa wa Polisi katika Wilaya ya Buikwe, Uganda, wanachunguza tukio ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 22 amepigwa na umeme hadi kufa.
Eunice Ajok alinaswa na umeme akiwa nyumbani kwake eneo la Lower Nava Zone, Manispaa ya Njeru, alipokuwa akifanya kazi zake.
Wakati wa tukio, mume wa Ajok Patrick Latigo ambaye ni fundi umeme alikuwa ameondoka kwenda kazini.
Akithibitisha tukio hilo, msemaji wa polisi mkoani humo, Hellen Butoto amesema kuwa Latigo aliunganisha waya wa moja kwa moja kutoka kwenye soketi, ambao ulipita chini ya kitanda cha wanandoa hao hadi kwenye sehemu ya kuoshea vyombo ya kutengenezwa ndani ya nyumba hiyo.
Polisi wanataka kubaini ni kwa muda gani Ajok amekuwa akiishi na fundi huyo wa umeme, na kama hakujali nyaya za umeme za moja kwa moja katika nyumba yao.
Mwili wa mwanamke huyo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Jinja kwa uchunguzi.