NSSF Yakaribisha Uamuzi Wa Ongezeko La Makato Ya Kila Mwezi
Shirika la Kitaifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekaribisha uamuzi wa Ijumaa iliyopita wa mahakama ya rufaa, kuruhusu kuathiri ongezeko la makato ya kila mwezi kama ilivyoainishwa na Sheria ya NSSF 2013.
Majaji watatu wa rufaa Hannah Okwengu, Mohamed Warsame na John Mativo walitofautiana na amri ya mahakama kuu mwezi Septemba mwaka jana, iliyotangaza sheria ya NSSF ya 2013 kuwa ni kinyume na katiba, ikitaja kutoshirikishwa kwa umma na kutokubaliana na seneti wakati wa mchakato wa kutunga sheria.
Awali, rais William ruto aliwahimiza washirika kutunga sheria upya ili kila mkenya anufaike uzeeni.
Kwa baadhi ya wafanyikazi ambao walikuwa wakikatwa shilingi mia .200 kila mwezi kama makato ya kisheria, mchango wao kwa NSSF utaongezeka mara kumi.
Wale wanaopata chini ya sh.elfu 15,000 kila mwezi, watahitajika kukatwa sh. 350 kwa mwezi. Wale wanaopata sh.elfu 15,000 watakatwa sh. 900 kwa mwezi, huku wale walio na mapato ya kila mwezi ya sh.elfu 18,000 na zaidi wakikatwa sh.elfu 1,080 kiasi ambacho waajiri wao watalingana.
Shilingi.elfu 3,000 zitakatwa kutoka kwa wale wanaopata angalau sh.elfu 50,000 kwa mwezi. Hili ni punguzo la asilimia 6 kwenye mapato yao ya kila mwezi, na mchango sawa na huo kutoka kwa waajiri, na kuifanya jumla ya asilimia 12 kwa mwezi.
Mwenyekiti wa bodi ya NSSF ametaja makato hayo mapya kuwa hatua muhimu na ushindi kwa wafanyikazi wa Kenya ambao unawawezesha kuimarisha akiba zao na kupata mustakabali wao wa kifedha na kuhakikisha kuwa wanastaafu kwa heshima.
Uamuzi wa mahakama ya rufaa unaongeza msukumo wa Rais William Ruto wa kuongezewa akiba ya wastaafu hadi angalau asilimia 25, kutoka asilimia 12 ya sasa.
Ongezeko hilo anasema litasaidia kuunda mfuko wa fedha ambazo serikali inaweza kukopa ili kugharamia maendeleo ya miundombinu kwa riba nafuu na kupunguza hamu ya nchi ya kukopa deni kubwa.