Home » Magavana Wa ODM Wakashifu Wabunge Wa Nyanza Kwa Kukutana Na Ruto

Magavana Wa ODM Wakashifu Wabunge Wa Nyanza Kwa Kukutana Na Ruto

Baadhi ya viongozi wanaoegemea chama cha Orange Democratic Movement (ODM) wamewakosoa wabunge tisa waliokutana na Rais William Ruto jana Jumanne.

 

Wakiongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo, viongozi hao wametaja ziara hiyo kuwa ya kibinafsi na wala haijaidhinishwa na chama cha ODM.

 

Mwenzake wa Kisumu Prof. Anyang’ Nyong’o ametilia mkazo suala hilo akisema wabunge hao walihudhuria mkutano huo bila kuidhinishwa na chama.

Chama cha ODM pia kimetoa taarifa kuhusu mkutano kati ya wabunge hao na Rais Ruto.

 

Wabunge hao wamedai mkutano huo ulilenga miradi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali.

 

Baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Elisha Odhiambo (GEM), Seneta wa Kisumu Tom Ojienda, Paul Abuor (Rongo), Caroli Omondi (Suba Kusini), Mark Nyamita (Uriri) na Gideon Ochanda (Bondo) phelix odwuor Jalang’o.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!