Home » Harmonize kupenda Tena

Swala la mapenzi limekuwa mtihani kwa mwanamuziki Harmonize na ameonesha nia ya kutokata tamaa.

 

Kupitia Instastory yake, Harmonize ameweka wazi kuwa kwa sasa hana hisia za kupenda tena licha ya wasichana wengi kutamani kuwa naye kwenye mahusiano.

 

Harmonize ameandika “Wanawake wengi wazuri wamejitahidi kunishawishi kupenda tena kwasababu wanajua ninapopenda nakuwa rafiki,mume, mtoaji na baba bora, nalikubali hilo. Lakini moyo wangu kwa sasa hauko tayari kupenda kabisa. Natumaini sitokuwa hivi daima. Niombeeni ili moyo wangu uweze kuruhusu kupenda tena”

Ikumbukwe Harmonize alitamba sana akiwa kwenye mahaba mazito na Jackline wolper ambaye kwa sasa ameolewa. Kabla ya hapo, konde boy amekuwa kwenye mahusiano na mwanamke mwenye asili ya kiarabu Sarah ambaye tetesi zilisema alichangia pakubwa mafanikio ya Harmonize kwenye muziki.

Harmonize amekuwa na Fridah kajala zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kutengana muda mchache kutoka na tuhuma za harmonize kuwa na mpenzi mwingine ambapo iliondokea mpenziwe kuondoka na kwa sasa Kajala yupo kwenye mahusiano ambapo hayajawekwa paruwanja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!