Vera Kuandaa Sherehe Kutambulisha Jinsia Ya Mtoto Wake Wa Pili

Mwanasoshalaiti na mwanamitindo nchini kenya Vera Mung’asia Shikwekwe almaarufu kama Vera Sidika amefichua kwamba tayari amepanga siku ya kujifungua mtoto wake wa pili.
Vera ameweka wazi kuwa atajifungua mtoto wa pili kwa njia ya upasuaji kama ilivyokuwa na mtoto wake wa kwanza.
Mpenziwe mwimbaji wa nyimbo za kibongo Fredrick Mtinda a.k.a Brown Mauzo alikuwa akiwashirikisha wafuasi wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram.
Alipoulizwa kuhusu jinsia ya mtoto ambaye amebeba tumboni kwa sasa, mwanasoshalaiti huyo alidokeza kwamba pia yeye na mumewe hawajapata kutambua huku akiahidi kuandaa hafla kubwa ya kufichua jinsia hivi karibuni.
Kulingana na Vera amefichua kuwa yeye na mume wake Brown Mauzo hawakupanga ujauzito wa mtoto wao wa pili pamoja.
Aidha, Vera Sidika amesema kuwa hana mpango wa kuongeza mtoto wa tatu wakati wowote hivi karibuni baada ya kujifungua.
Mwanasoshalaiti huyo pia ameeleza kwamba sababu ya yeye kutoweka kwenye mitandao ya kijamii kwa muda ni kwa kuwa amekuwa akihusika katika utayarishaji wa kipindi cha Real Housewives of Nairobi.