KPLC Yatangaza Kupotea Kwa Umeme Nairobi
Kampuni ya Kenya Power KPLC, imetangaza kuwa maeneo 43 jijini Nairobi yatakatizwa na umeme kufuatia utaratibu wa marekebisho uliopangwa kufanyika leo hii Jumanne, Februari 7.
Katika notisi, kampuni hiyo imeonyesha kuwa baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya marekebisho yatakosa umeme kwa saa 3 huku mengine yakikatika kwa saa 8.
Baadhi ya maeneo yatakayokumbwa na ukosefu wa umeme kwa saa nane ni pamoja na maeneo yanayozunguka Kitsuru kama vile Kitsuru Ridge Villas estate, Kitsuru Country Homes, eneo la Kihara, Old Karura Rd, Soko la Kihara, White Cottage School, Weaverbird Kenya, Sehemu ya Kirawa Rd, Hotani Close. na Taasisi ya Parazoro.
Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza saa 9 asubuhi.
Maeneo karibu na barabara ya Redhill pia yamejumuishwa katika marekebisho yaliyopangwa.
Kenya Power imeongeza kuwa baadhi ya maeneo ya Nyari, Ubalozi wa Uswizi, Gachie, Kanisa la Karura SDA, Shule ya Sekondari ya Hospital Hill, Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE), Trio Est, Redhill Rd na Rosslyn Green yatakabiliwa na tatizo hilo kwa saa 8.
Maeneo mengine ya Nairobi ambayo yataathiriwa na hitilafu hiyo ya saa 8 ni pamoja na Umoja Innercore yenye maeneo muhimu yalikayoathiriwa kama vile Shule ya Cathsam, Innercore Sango, Ofisi ya Kwa Chief Umoja, Soko la Umoja 2, Hoteli ya Oloibon na Shule ya Msingi ya Unity.
Kwa upande mwingine, Thigiri Groove, Thigiri Ridge, Mafunzo ya NSIS, na Brookside Drive zitakatizwa kwa saa tatu (kuanzia 9 asubuhi hadi 12 jioni).
KPLC imeongeza kuwa Rosslyn Close, Thigiri Farm, Nyari Est, Rosslyn Heights Est, Redhill Drive na wateja wa karibu pia watarejeshewa umeme wao wa kawaida baada ya kukamilika kwa marekebisho saa 12 asubuhi.
Hata hivyo, licha ya Nairobi kuathiriwa zaidi na marekebisho hayo yaliyoratibiwa, kaunti zingine kama vile Siaya, Kitui na Busia zinatazamiwa kukumbwa na hitilafu hiyo ya umeme.
Maeneo yatakayoathiriwa ni pamoja na Butula huko Busia na maeneo ya karibu huko Hono, kaunti ya Siaya.