Hakuna Mkenya Aliyeripotiwa Kufa, Kujeruhiwa Kule Uturuki na Syria
Katibu mkuu wa Umma wa Masuala ya Diaspora Roseline Njogu ametangaza kuwa hakuna Mkenya yeyote ambaye ameripotiwa kujeruhiwa au kufa katika tetemeko la ardhi lililotokea mapema jana Jumatatu nchini Uturuki na Syria.
Njogu amebainisha kuwa hakuna Mkenya ambaye ameripotiwa kujeruhiwa na Ubalozi wa Kenya nchini Uturuki na ametoa nambari za simu ya dharura ambayo Wakenya wanaweza kuwasiliana nao.
Pia ametuma risala zake za rambirambi kwa familia na marafiki wa waathiriwa wa mkasa huo.
Kufikia leo hii Jumanne, takriban vifo elfu 4,372 vimethibitishwa baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu kutikisa mataifa hayo mawili.
Mkuu wa huduma za umma Uturuki Yunus Sezer amethibitisha kuwa idadi ya waliofariki Uturuki iliongezeka hadi elfu 2,921 na jumla ya elfu 15,834 waliripotiwa kujeruhiwa.
Sezer ameongeza kuwa angalau majengo elfu 2,834 yaliharibiwa, na mamlaka ilitoa makazi kwa raia usiku kucha.
Nchini Syria, vifo elfu 1,451 na majeruhi elfu 3,531 vimeripotiwa na maafisa