Home » Uza Mali Yangu Ikiwa Sijalipa Ushuru, Asema Mama Ngina Kenyatta

Uza Mali Yangu Ikiwa Sijalipa Ushuru, Asema Mama Ngina Kenyatta

Kwa mara ya kwanza, Mke wa Rais wa zamani Mama Ngina Kenyatta amezungumza dhidi ya kile alichokitaja kuwa siasa zisizo na maana za masuala ya ushuru.

 

Katika matamshi yake, ameonyesha wazi mzozo wa hivi majuzi wa kisiasa unaoshutumu familia yake kwa kutolipa ushuru, Mama Ngina amesema wanasiasa wanaendeleza madai ya uwongo ili waonekane wanafanya kazi.

Mama Ngina amesema masuala ya ushuru yanaweza kushughulikiwa kupitia njia za serikali na ikihitajika mahakama za sheria, akiongeza kuwa mikutano ya hadhara haina nafasi katika masuala ya ushuru.

Mkewe Rais wa zamani amezungumza alipokuwa akiwahutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa Kanisa Katoliki la Tewa ambalo alisaidia kujenga eneo la Mpeketoni, Kaunti ya Lamu.

Kadhalika, Mama Ngina amedai serikali kupiga mnada mali yake ili kulipa deni lolote analohisiwa ikiwa ni kweli kwamba amekuwa halipi kodi yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!