Home » Walimu Wa Chekechea Wasusia Pendekezo La SRC

Muungano wa Walimu wa Elimu ya Awali nchini (KUNOPPET) umepinga pendekezo tata la Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) kuagiza magavana wa kaunti kuwalipa walimu wa Elimu (ECDE) mishahara ya chini ya kila mwezi.

 

Katika mapendekezo ya SRC, walimu wa chini wa ECDE (ECDE wanapaswa kulipwa kima cha chini cha mshahara wa shilingi elfu .7,836 na kima cha juu zaidi kikiwa shilingi elfu .8,717, huku mwalimu wa juu zaidi wa ECDE akipata shilingi elfu .15,224.

 

Akihutubia wanahabari, mwenyekiti wa KUNOPPET Lawrence Otunga amesema kuwa hawatakubali walimu wa shule ya chekechea kudharauliwa na kudhalilishwa kupitia kupata mishahara duni na wanapaswa kutendewa haki kama watumishi wengine wa umma.

 

Otunga ameapa kupigania kurekebishwa kwa pendekezo la mishahara hadi pale uamuzi unaofaa utakapoafikiwa.

 

Mwenyekiti Otunga amewashutumu Magavana dhidi ya kutekeleza maagizo ya SRC, akisisitiza kwamba malipo yaliyopendekezwa hayawezi kusaidia mtu yeyote kutokana na vizingiti vya sasa vya kiuchumi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!