Home » Azimio Yapuuza Hatua Ya Wakili Wa Chebukati

Huku madai ya kiongozi wa Azimio La Umoja One-Kenya Raila Odinga kwamba makamshina wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, walimtembelea nyumbani kwake kabla ya matokeo ya uchaguzi yakiendelea kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wakenya, sasa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amepuuzilia mbali madai ya wakili wa mwenyekiti wa tume hiyo Steve Ogolla kumpa kiongozi wao makataa ya siku saba kutoa video hiyo.

Sifuna amesema kuwa hakuna kitakachomzuia wakili Steve Ogolla kumwakilisha mwenyekiti mstaafu wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC Wafula Chebukati, dhidi ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

Sifuna kupitia akaunti yake ya twitter amesema kuwa “ila kwa ada za kisheria, hakuna kitu kingine kitakachotoka kwenye tukio hilo la kisheria”.

Haya yanajiri baada ya wakili Steve Ogolla kutoa barua ya kumtaka Raila kutoa ushahidi wa ziara ya mwenyekiti huyo wa zamani nyumbani kwake ndani ya siku saba.

Ogolla alitishia kumshtaki Raila, kwa niaba ya Chebukati, kuhusu kauli yake wakati wa mkutano wa Jumapili wa Jacaranda ambapo alidai kuwa Chebukati na makamishna wa zamani Abdi Guliye na Boya Molu walimtembelea nyumbani kwake kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Kiongozi huyo wa Azimio pia alidai makamishna hao walimwomba kitu fulani na kwamba ana ushahidi madai ambayo Chebukati amekanusha.

 

Wakati huu, Odinga anahudhuria Kongamano la 14 la Uongozi mjini Abuja nchini Nigeria, ambako ameweka bayana kuwa teknolojia katika uchaguzi inaweza kutumiwa kuwanyima wananchi haki yao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!