Mahakama Uganda Yaamuru Mwanamke Kumlipa Ex Kwa Talaka
Mahakama nchini Uganda imeamuru mwanamke kumlipa mchumba wake wa zamani (EX) zaidi ya Ksh. 348,491 kwa kuvunja uchumba wao baada ya kumlipia masomo, ikisema kuwa alisababisha “usumbufu na uchungu wa kisaikolojia”.
Kulingana na hati za mahakama mwalimu mstaafu Richard Tumwiine, 64, alimlipia Fortunate Kyarikunda diploma ya sheria wakati wanandoa hao walikuwa wanachumbiana.
Mwanamke huyo anayesemekana kuwa na umri wa miaka thelathini – baadaye “alimgeuka Richard akisema hawezi kuolewa na mzee”.
Jaji amesema Kyarikunda atalazimika kurejesha shilingi 9,439,100 za Uganda (dola 2,560) ambazo Tumwiine alitumia katika masomo yake.
Tumwiine amedai kwamba kesi hiyo imeacha majeraha ya kudumu moyoni mwake.
Lakini waziri wa zamani wa maadili wa Uganda na mwanaharakati mashuhuri wa haki za wanawake Miria Matembe alikosoa uamuzi wa “upande mmoja”.