NACADA Kuanza Harakati Za Kudhibiti Pombe Na Mihadarati

Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni dhidi ya Unywaji Pombe na Dawa za Kulevya (NACADA) imetangaza mipango ya kuzidisha vita dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya nchini.
Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa NACADA Kasisi Stephen Kiptoem Mariori amesema mamlaka hiyo itashirikisha Serikali za Kaunti na washikadau wengine ili kushirikiana katika kutafuta suluhu la changamoto za utumizi wa dawa za kulevya nchini.
Kiongozi wa huyo mpya wa NACADA ambaye aliteuliwa na Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa mamlaka hiyo kufanya kazi na Maafisa wa Utawala wa Kitaifa wa Serikali na washikadau wengine katika kuhakikisha kuwa Sheria ya Kudhibiti Vinywaji Vileo 2010 inatekelezwa madhubuti ili kudhibiti viwango vidogo, bidhaa ghushi na magendo na aina yoyote ya vileo ambavyo havijaidhinishwa ambavyo vinahatarisha maisha.