Home » Cindy Sanyu Atangaza Kurudi Kwenye Muziki

Msanii aliyepotea kwa muda mrefu na mkongwe nchini Uganda Cindy Sanyu ametangaza kurudi kimuziki baada ya likizo ya miaka zaidi ya miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amedhibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba ana mpango wa kuingia studio mwezi ujao kwa ajili ya kurekodi wimbo wake mpya.

Hata hivyo, amewataka mashabiki zake kupendekeza mada atakayoimba kwenye ngoma yake ijayo ambayo kwa njia moja au nyingine italeta tija kwenye maisha yao.

“Naingia studio kurekodi wimbo mpya mwezi ujao. Una mada yoyote unayodhani ninapaswa kuzingatia ambayo itabadilisha maisha yako kama shabiki? #walkwithme,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Utakumbuka 2021 Cindy alitangaza kuchukua mapumziko mafupi kwenye muziki wake kwa ajili ya kupata muda mzuri wa kukaa na familia yake.

Msanii huyo aliahidi mashabiki zake kuwa atarejea kwenye shughuli za kimuziki muda sahihi utakapowadia na tangu kipindi hicho hajaachia wimbo wowote.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!