Home » NTSA Yawataka Madereva Kuzingatia Hatua Za Usalama Barabarani

NTSA Yawataka Madereva Kuzingatia Hatua Za Usalama Barabarani

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama barabarani NTSA imewataka madereva wote wa magari kuhakikisha usalama wa watoto shule zinapofunguliwa.

Katika taarifa yake NTSA imeonya kuwa msimu wa kurejea shuleni hapo awali umerekodi ukiukaji wa sheria unaosababisha vifo na majeraha mabaya.

Mamlaka hiyo pia imewataka wazazi kutumia njia salama za usafiri kuwasafirisha watoto kwenda na kurudi shuleni ikisema ni magari yanayokidhi mahitaji na yanayostahili na hivyo basi yafaa wawe makini.

Aidha NTSA pia imewashauri wazazi kutumia NTSA Mobile App inayopatikana kwenye Play store ili kuthibitisha magari yanayofaa kuwa barabarani kwa kunasa nambari ya usajili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!