‘Walitaka Tutangaze Raila,’ Abdi Guliye Asema

Wakenya wa mirengo mbalimbali za kisiasa wanaendelea kufurika katika mitandao ya kijamii na kutoa hisia zao kinzani kuhusiana na taarifa aliyotoa jana wakati wa mahojiano aliyekuwa kamshina wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Abdi Guliye kwamba kulikuwepo na watu fulani waliotaka Raila odinga atangazwe mshindi.
Baadhi ya wakenya wa mrengo wa azimio la umoja one-kenya wanadai tume ya IEBC ingekubali kuonyesha data za uchaguzi ndipo wao pia waridhike na matokeo na wala si kubana huku wale wa mrengo wa Kenya kwanza wakiendelea kulaumu wana-azimio kwa kutokubali matokeo ya uchaguzi kila mwaka.
Guliye akitoa ushahidi mbele ya mahakama inayoongozwa na Jaji Aggrey Muchelule alidai kwamba mnamo Agosti 15, mwaka jana, saa chache kabla ya kutangaza matokeo ya mwisho ya urais, timu ya wageni wanne ilidai kuhudhuria pamoja na makamishna wote mwendo wa saa 10:00 asubuhi.
Kadhalika Guliye alisema kuwa timu hiyo ya watu wanne ilitambulishwa, na wakasema kwamba walikuwa hapo kwa niaba ya Kamati ya Ushauri ya Usalama wa Kitaifa (N.S.A.C).