Home » Waliolipa Mahari Kwa Akaunti Za Shule Walia

Mahari kamwe hailipwi kwenye akaunti za shule. Mahari hupewa baraza la wazee wa binti na yalipao kwenye akaunti za shule, hesabu kama hisani.

Alfred na Juma japo si majina yao halisi, mioyo ya utu na huruma iliwasukuma kujaribu bahati ya kuwafadhili Maria na Salome. Wote hawa, Maria na Salome walikuwa wenye ari ya kusoma japo, uchechefu wa karo ndio ulikuwa tatizo kwao.
Maria kwa kuwa alifiwa na wazazi wake halali, Alfred alijihimu kumsomesha hadi chuo kikuu naye Salome, familia yake maskini haikumpa nafasi ya hata kupata sodo wakati wa hedhi seuze karo ya shule? Kwa Salome, maisha ya ukata yalimkutanisha na Juma mwana bodaboda aliyeacha shule akiwa darasa la saba.
Kila wakati, Juma alijizatiti kumsaidia Salome kama mzazi japo walikuwa washindania miaka minne. Kwa kusaidiwa na Juma, Salome alifanikiwa naye hadi kufika chuo kikuu. Wote hawa, Maria na Salome kwa kufika chuoni, wafadhili wao wa rika lao ” Alfred na Juma”, waliamua kutingiza viberiti kama njia ya kuhalalisha mahusiano wawe kama wapenzi.
Kwa mshtuko, posa zao zilikataliwa na mabinti hawa. Wanaume wakalia kwikwi kwa “kusalitiwa”. Aimbavyo Freshly Mwamburi, “kama ni wewe ungefanya nini?” Wanaume, zindukeni kutoka usingizini. Mahari hayalipwi kwenye akaunti za shule. Mahari hupewa baraza la wazee wa binti na, yalipwapo kwenye akaunti za shule, hesabu kama hisani.
Ukimsaidia binti karo ya shule au mahitaji yoyote, mwanaume kamili hastahili kutarajia “malipo” kwa njia yoyote ile iwapo hamna maagano. Tenda wema nenda zako lakini, mahari hayalipwi kwenye akaunti za shule.
Kwa mabinti, kumbukeni mlikotoka. Iwapo uliahidiana na mtoto wa mtu kuwa akufadhili kisha mtaoana, usivunje ahadi baada ya kuona mwanga. Mali na pesa, ni maua ya dunia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!