Home » Nick Salat Azungumzia Masaibu Yake Ndani Ya Chama Cha KANU

Nick Salat Azungumzia Masaibu Yake Ndani Ya Chama Cha KANU

Katibu Mkuu wa Chama cha KANU Nick Salat amefunguka kuhusu matatizo yake na chama hicho kinachoongozwa na aliyekuwa Seneta wa Baringo Gideon Moi, matatizo ambayo yalisababisha kusimamishwa kwa uanachama wake kwenye chama hicho.

Barua kutoka kwa Moi tarehe 15 mwezi jana ilidai kwamba Salat alisimamishwa kazi kwa sababu ya madai ya utovu wa nidhamu na ukiukaji wa katiba ya chama.

Salat sasa amedokeza kwamba chanzo cha kusimamishwa kwake chamani ni  maswali aliyoibua wakati wa mkutano wa KANU uliofanyika Nakuru, ambapo inadaiwa alipinga uongozi wa Moi na kutaka wote wanaoshikilia nafasi chamani akiwemo yeye kujiuzulu kufuatia kushindwa kwa chama hicho kutwaa viti vingi kwenye uchaguzi wa  Agosti mwaka jana.

Katika mahojiano na jarida moja la hapa nchini, Salat alidokeza kwamba kinyume na inavyosemekana ameuza mali ya chama, hayo ni madai yasiyo na msingi wowote.

Wakati huo huo, amesema yuko tayari kufika mbele ya uongozi wa chama hicho kujitetea hata kama atafukuzwa chamani ili kusafisha jina lake machoni pa umma.

Akizungumza katika hafla moja na rais William Ruto kule Bomet hii leo, Salat ametangaza kwamba sasa anahama KANU na kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!