Home » ”Nimechoka Kuwa Single”Chege Chigunda

Msanii wa Bongo Flavour Chege Chigunda

Msanii wa BongoFleva, Chege Chigunda amechoka maisha ya kuwa SINGLE, ametangaza hadharani kuwa anahitaji mwanamke wa kufunga naye ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chege amedokeza kuwa japo anatarajia ndoa lakini bado hajapata mwanadada wa ndoto yake ikizingatiwa kuwa ndoa sio ya mtu mmoja bali ni ya watu wawili; mke na mume.

Hitmaker huyo wa “Wacha Waoane” amewataka wanawake wote ambao wanajiona kuwa na nafasi ya kuwa mke halali kwake kujiongeza huku akisema kuwa wanaume wanahitaji mambo machache sana kutoka kwa wanawake.

“Wanadada jiongezeni wanaume tunahitaji mambo machache sana,mfano mie Ukinipenda, Ukiniheshimu, Ukiniskiliza tu basi. Naoa mwaka huu huu 2023 chap,” Chege aliandika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!