Home » Tanasha Agadhabishwa na Lebo Yake

Aliyekuwa mkewe msanii kutoka bongo fleva Diamond Platinumz Tanasha Donna, ameudhika na kuichana lebo yake kwa kile anachodai kwamba imeachia wimbo wake mpya bila ridhaa yake.

Kupitia mfululizo wa Instastory zake kwenye mtandao wa Instagram, Tanasha ameshangazwa na kitendo cha Ziiki kuachia ngoma hiyo bila ya makubaliano yoyote kwa kigezo kuwa haikuwa imefikia ubora uliohitajika na uongozi wa lebo hiyo.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/13/sipendi-waafrika-nataka-kuolewa-na-mzungu-huddah-monroe-asema/

Mrembo huyo amesema kwamba amechoshwa na manyanyaso ambayo ameyapitia chini lebo hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa huku akitishia kuichukulia Ziiki hatua kali za kisheria ili dunia ione udhalimu wake.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/10/simu-nyingi-ni-ngono-nyingi-aonya-justina-syokau/

Hata hivyo, amemalizia kwa kusema iwapo lebo hiyo ingekubali wamalize tofauti zao nyuma ya pazia,  hangeanika malalamiko yake kwenye mitandao ya kijamii lakini kutokana na ujeuri wao ameamua kuweka wazi ghadhabu zake.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!